Adhabu ya kinyama kwa mwanamke India
OnAdhabu ya kinyama kwa mwanamke India |
Uso wa mwanamke huyo ulikua umepakwa rangi nyeusi wakati alipokuwa akiadhibiwa.
Polisi inawashikilia watu takriban thelathini wakihusishwa na tukio hilo la kumdhalilisha mwanamke huyo mwenye umri wa miaka arobaini na mitano,tukio lililotokea baada ya mwanamke huyo kushutumiwa kumuua binamu yake.
Familia ya mwanamke huyo iliuchoma mwili wa binamu aliyedaiwa kuuawa na mwanamke huyo kabla ya kutoa taarifa kwa polisi.Afisa katika jimbo la Rajasthan wamesema kuwa ni kinyume cha sheria kwa baraza hilo kutoa hukumu ya namna hiyo.
Maoni
Chapisha Maoni