Mamlaka za vijiji na kata zifuate taratibu

Viongozi wa serikali za kata na vijiji wametakiwa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kuleta tija na kuondoa minong’ono isiyokuwa na sababu toka wananchi hali ambayo huweza kusababisha kudumaa kwa maendeleo.


Hayo yamesemwa na Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya kibondo mkoani kigoma  Bw Dominick Luhamvya wakati warsha ya kujadili miongozo na kanuni za serikali za mitaa ambaye alikuwa alikuwa mwezesha katika warsha ilihiyofanyika  wilayani kibondo.

Bw.luhamvya amesema kuwa katika kuweka utaratibu mzuri wa kiuongozi haina budi viongozi kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi wakizingatia haki katika kuwaboreshea miundomnbinu ikiwemo maji,barabara,na shule, ilikuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii kuwa nzuri.


Aidha amesema kuwa baada ya watendaji wa kata na vijiji sambamba na madiwani kufanya mikutano na wananchi na mupata kelo mbalimbali kutoka kwa wananchi wataziwasilisha katika balaza la madiwani ambao ndio wenye kikao cha maamuzi.

Katika warsha hiyo baadhi ya madiwani ambao ni Hadija Maulidi viti maalum na Cleophace kata ya kizazi  walipata nafasi ya kutoa michango yao mbalimbali hususa swala la maadili kwa madiwani na watumishi wa halmashauri ihusianayo na utendaji kazi hali itakayo saidia katika hali ya kutatua migogoro mbalimbali itokayo kwa wananchi na  hatimaye kuwepo usawa wa kimaendeleo.


Hata hivyo baadhi ya wananchi wamepata nafasi ya kutoa maoni mbalimbali wakati wakizungumza na gazeti hili, wamesema kuwa viongozi wengi wa ngazi za kata na vijiji wamekuwa wakijisahau kutowashirikisha wananchi kwa kutoitisha mikutano ambayo inatmbulika kisheria badala yake ucha maeneo yao kuwa kama vile yametelekezwa kwawananchi kutofahama kilichopo juu ya maendeleo ya vijiji vyao.

Aidha wamesema kama viongozi watafuata taratibu kanuni na miongozo ianayotakiwa, hali hiyo itakuwa bora kwa wananchi kwani itasaidia na wao kuwa katika hali nzuri ya kimaendeleo  na kufahamu namna ya utendaji kazi kutoka kwa viongozi wao.

Kikako hicho kilijikita  kujadili rasmu ya sheria na kanuni za miongozo ya mikutano ya serikali za mitaa hususa vikao vya madiwani kwa kutumia kanuni mpya za hi visasa tofauti na zile za zamani ambapo madiwani hao watafanya vikao vitatu kwa mfululizo kwa kutoa taarifa za kila kata kulingana na wananchi watakavyokuwa wametoa maoni kwenye mikutano huko vijijini baadae kutoa uamuzi 

    Katika kanuni ya zamani ilikuwa ni siku mbili hali iliyowabana madiwani hao kutokutoa taarifa za kata zao tena si kwa kina hali inayosababisha kuongezeka kwa migogoro isiyoisha kwakuwa haijadiliwa na kutatuliwa.

Mwaisho



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao