NHIF yajenga kituo cha kisasa cha kuchunguza magonjwa Dodoma

SERIKALI kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), imejenga kituo kikubwa cha kisasa cha uchunguzi wa magonjwa mbalimbali mkoani hapa ili kuokoa fedha zinazotumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi.
Kituo hicho kilichojengwa ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kinatarajiwa kuanza kazi Januari mwakani.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea kituo hicho jana, Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Shabaan Mlacha, alisema kituo hicho kilichogharimu sh bilioni 36 ni matokeo ya kukipanua chuo hicho ambacho kwa sasa ndicho kikubwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
“Kituo hiki kilikuwa kijengwe mjini Dodoma, lakini kimejengwa hapa kwa agizo la Rais na hii yote ni kukifanya chuo hiki kuwa kikubwa katika ukanda huu wa Afrika,” alisema Prof. Mlacha.
Alisema madaktari wengi watakaokuwa katika chuo hicho watatoka Kitivo cha Tiba na Afya kilichopo katika chuo hicho na kwamba, mwaka jana wameshatoa Shahada ya kwanza ya Udaktari.
Aliongeza kuwa, baada ya kituo hicho kuanza kazi mwakani, itakuwa ni fursa nyingine ya kuanza ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa ambalo litaweza kulaza wagonjwa wapatao 300 na kwamba, tayari wamepata msaada wa vifaa kutoka Japan.


Mshauri mwelekezi wa kituo hicho, Habib Nuru, alisema jengo la kituo hicho lenye ghorofa tatu, litakuwa na vitengo na madaktari wa magonjwa mbalimbali ikiwemo sehemu ya wagonjwa wa dharura wanaotokana na ajali za barabarani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao