Wanafunzi wa shule ya msingi walalmikia kufanyishwa kazi za watu Binafsi mitaani na Walimu
fred eliasafu kaimu mkurugenzi Halimashauri W kibondo |
Wanafunzi shule ya msingi Shunga |
Joseph John mkuu wa shule ya msingi Shunga |
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Shunga iliyoko katika
kijiji cha Kumuhama kata ya Bitare wilayani kibondo mkoani kigoma wamelalamikia kitendo
cha kufanyishwa kazi za watu binafsi kama kusomba matofari , kabeji na miwa
kisha walimu kuchuka pesa baada ya wanafunzi kufanya kazi kwa kwa madai kuwa ni za matumizi ya shule
Baadhi ya wanafunzi hao wakiongea na na cliouds Tv kijijini
hapo wamesema kuwa wameporomoka
kitaaruma kutokana na kufanyishwa kazi
za kubeba matofari ya wananchi , kabeji na miwa kisha pesa kuchukuliwa na waalimu wa shule
hiyo ambapo wamekuwa wakiambiwa kuwa zinaingia kwenye mfuko wa shule
Mkuu wa shule ya msingi shunga bw Joseph John nilimkuta
shuleni hapo na alipoulizwa kuhusu swala hilo
amekili wanafunzi kutumikishwa katika kazi hizo na kwamba
waliamua kufanya hivyo ili kupata hela ya kumlipa mlinzi ili kulinda madawati
mapya waliyoletewa na serikali na kwamba wazazi wamekuwa wakikaidi kuchangia
pesa pale inapobidi
Baadhi ya wazazi waliopata kuzungumza na clouds katika
kijiji cha kumuhama wamesema kuwa kitendo si kuzuri kwani wapo baadhi ya
wanafunzi ambao afya zao haziridhishi hivyo ili zipo kazi ambazo hata wakiwa
majumbani kwao uwa hawazifanyi na kutegeana na hali halisi ilivyo kwa
mwanafunzi
Aidha wazazi hao wamesema kuwa hawajashilirikishwa katika swala hilo lakini
pamoja na hayo wamekuwa wakitoa mchango wao pale inapobidi na kudai kuwa kama kuna tatizo katika swala la
uendeshaji wa shule walimu husika wanatakiwa kupeleka katika uongozi wa
serikali ya kijiji au kuitisha mkutano wa wazzi ili kujadili lakini mambo hayo
hayafanyiki
Kwa upande wake
mratibu elimu wa kata ya bitare Bi
ISABERA NYUMAYINZU amesema kuwa wanaopaswa kuwajibika katika maswala ya
kuwalipa walinzi na matumizi mengine ya shule ni wazazi kwa kushirikiana na
uongozi wa kijiji na si wanafunzi
nae kaimu mkurugenzi wa halmashauru ya wilaya ya kibondo bw
Fed Eliasafu amesema kuwa si utaratibu wanafunzi kufanyishwa kazi kwa watu
binafsi na kwamba atalifanyia kazi na hatua sitahiki zitachukuliwa
Maoni
Chapisha Maoni