Bunge la Ufaransa lajadili kuhusu taifa la Palestina

Moja ya agenda ya kikao cha Bunge la Ufaransa ambalo linakutana Ijuma wi hii hii ni kulitambuwa taifa la Palestina, kabla ya kupigia kura uamzi huo utakaochukuliwa katika kikao hicho. Kura itapigwa Desemba 2 mwaka 2014.

Kura hiyo ya ishara haitobadili msimamo rasmi wa Ufaransa. Vikao kama hivyo vya Bunge vimekua vikifanyika katika nchi nyingi barani Ulaya na kupitisha uamzi wa kulitambua taifa la palestina, hali ambayo imekua ikiwapa motisha na faraja raia wa Palestina.
Pendekezo la azimio ambalo litajadiliwa na Bunge Ijumaa wiki hii, “ limeitolea wito kwa serikali ya Ufaransa kulitambua taifa la Palestina”. Wito ambao hauna madhara yoyote kwa msimamo wa Ufaransa, ambayo inabaini kwamba muda haujawadi Palestina kuwa taifa. Ufaransa inaona kwamba mazungumzo kati ya Israel na Palestina ndiyo yatapelekea kuundwa kwa taifa la Palestina.
Jitihada za Wabunge na Maseneta wa Ufaransa ni ishara yenye nguvu kwa jumuiya ya kimataifa
Qassem Barghouti, mwanae kiongozi wa mamlaka ya Palestina, alibaini hivi karibuni kwamba jitihada za Wabunge hazitobadili chochote msimamo wa Ufaransa.
“ Nadhani kwamba jitihada hizi zinazofanywa na Wabunge wa Ufaransa na wale kutoka nchi mbalimbali za Ulaya, ni muhimu na zinawafariji raia wa Palestina kwamba wabunge kutoka mataifa mbalimbali barani Ulaya wanawaunga mkono, kwa sababu katika kila nchi, Bunge linawakilisha raia”, alisema Qassem Barghouti.
Hivi karibuni Sweden ilichukua uamzi wa kulitambua taifa la Palestina. Sweden ni nchi ya kwanza barani Ulaya kulitambua taifa la palestina.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji