Kukwama kukamilika miradi ya maendeleo fedha za serikali kuchelewa
Kukwama kukamilika miradi ya maendeleo fedha
za serikali kuchelewa
Halmashauri
ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma inakabiliwa na changamoto ya kutokukamilika
kwa miradi ya maenedeleo hususa ni katika miradi ya Maji Elimu na afya kwa
sababu ya kuchelewa kwa wakati fedha za bajeti zinazokuwa zimetengwa na
serikali kuu
Hayo
yamesemwa na Madiwani wakati wa kikao cha Baraza kilichofanyika wilayani
humo,Madiwani hao, wamesema kuwa kuchelewa kufika fedha hizo kumesababisha kutokukamilia kwa
ujenzi wa miradi mbalimbali na kuwafanya wananchi wanaokuwa wamechangia nguvu
zao kukata tamaa
Aidha
wamesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2014/2015 halmashauri hiyo ilidhinishiwa kiasi cha shilingi billion 1.8 lakini hadi
September 15 2014 fedha hizo zilikuwa bado hazijafika hali inayosababisha
miradi mingi kubaki viporo huku wananchi wa maeneo husika wakikata tamaa na kuto kuitikia kwa nguvu tena katika
muendelezo wa miradi hiyo
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Juma Maganga amesema kuwa kinachokwamisha miradi mingi ya
maji iliyoko wilayani kakonko
inasimamiwa na halmashauri ya Kibondo kwakuwa hapo mwanzo ilikuwa wilaya moja na
kugawanywa hivi karibuni na kuwataka
madiwani kutingiza mambo ya siasa kwenye maswala ya maendeleo kwakuwa kila kitu
kiko wazi
Nao
wananchi waliohudhulia kwenye Baraza hilo
wamedai kuwa miradi mingi uwa inaelekezwa vijijini na washiriki wakubwa katika
uchangiaji wa ujenzi huo ni wanavijiji nao wanakabiliwa na ukosefu kipato
katika familia hivyo wanapojitoa na kisha kuona kile walichokuwa wanakiangaikia
kinakwama ukata tama kabisa na kutotaka kushiriki wakati mwingine.
Hata
hivyo, wananchi hao wamesema hali hiyo usababisha kukosekana kwa huduma stahiki
kama kukosa elimu bora Afya na Maji safi
na kuleta usumbufu, na kuiomba serikali kuongeza raslimali fedha kwa wakati ili
kuleta ufanisi na maendeleo yanayokuwa yamekusudi katika miradi husika
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni