Mkutano wa G20 wakamilika
Waziri mkuu nchini Australia Tonny Abott amefunga mkutano wa mataifa tajiri duniani G20 akieleza kwa kina ahadi za kiuchumi zilizoafikiwa na viongozi wa dunia kwenye mkutano huo.
Amasema kuwa ikiwa ahadi hizo zitatekelezwa hatua hiyo itaupa msukumo uchumi wa dunia katika miaka mitano kwa asilimia 2.1.
Bwana Abbott amesema kuwa mabadiliko hayo pia yatabuni mamilioni ya ajira.
Pia amezungumzia kuhusu mipango ya kuongeza nafasi za wawawake kwenye ajira na njia za kuyazuia makumpuni ya kimataifa yanayokwepa kulipa ushuru.
Rais wa Marekani Barrack Obama alifanya mikutano na viongozi wa Australia na Japan kando ya mkutano huo ambapo waliaidi kuendelea kuwa na ushirikiano wa kijeshi.
Owaziri mkuu wa Australia Tony Abottngeza kichwa |
Maoni
Chapisha Maoni