Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameyashutumu mataifa ya magharibi kwamba yanataka kubadilisha serikali ya Urusi kwa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi, kwa sababu ya mzozo wa Ukraine.
Aliuambia mkutano wa wataalamu wa mashauri ya nchi za nje mjini Moscow kwamba mataifa ya magharibi siyo yanataka kuifanya Urusi ibadilishe sera zake kuhusu Ukraine tu, bali yanataka kubadilisha serikali ya Urusi.
Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Urusi vikwazo kadha vya kiuchumi kwa sababu zinaishutumu kuwa inawasaidia wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine.
Maoni
Chapisha Maoni