Watanzania watakiwa kupima afya zao

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Seif Rashid, amewataka Watanzania kujijengea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara badala ya kusubiri wafikie dalili za ugonjwa hatua mbaya.
Dk. Rashid, alisema hatua hiyo itawawezesha kupata matibabu mapema kabla ya kusababisha madhara makubwa.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina ya afya kwa wabunge iliyoendeshwa na kituo cha afya cha Agakhan Bungeni jana, Dk. Rashid alisema kuwa watanzania wakijijengea tabia ya kupima wataepushwa na vifo visivyo vya lazima.
"Magonjwa mengi yamekuwa yakianza taratibu, ndani kwa ndani, hivyo kama wananchi wakijenga tabia ya kupima afya angalau mara moja kwa mwezi na kupunguza kula vyakula ambavyo wataalamu wa afya wanakataza, itaepusha vifo vya ghafla vinavyotokea,” alisema na kuongeza.
Tujitahidi kupunguza vyakula kama nyama choma, chumvi nyingi, itasaidia kuepusha matatizo yanayotukumba kama kisukari, shinikizo la damu na uzito kuzidi kupita kiwango cha urefu wa mtu.
"Kumekuwa na tatizo la watu kuanguka au kufa ghafla, hii inatokana na watu kutokupima na kujua afya zao, ukijua kinachokusumbua ni rahisi kuishi miaka mingi kwa kufuata masharti,” alisema.
Waziri huyo, alisema kwa mwaka 1996, asilimia 42 walifanyiwa vipimo na kugundulika wana vimelea vinavyosababisha magonjwa yasiyo na tiba.
Kwa upande wao wabunge waliohudhuria semina hiyo, wengi wao wamefurahia kupata nafasi hiyo ya kupima magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na uzito ili kujua hali ya miili yao, kwani wanakuwa na shughuli nyingi na kushindwa kufuatilia afya zao.
Naye Meneja wa Agakhan, Mustapha Bapumia, alisema hospitali hiyo imeamua kuwapima wabunge hao ili kujua afya zao na kuanza masharti ya vyakula na dawa mapema wanapogundulika na magonjwa hayo.


Alisema hospitali hiyo ina mpango wa kujenga matawi katika mikoa mbalimbali, ambako kila miezi mitatu watatoa kituo kimoja na ndani ya miaka miwili watakuwa wamejenga vituo 30.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao