Watanzania tulieni katika kipindi hiki cha mgawanyiko sababu Escrow
Mwemezi Muhingo Mwanachi
Watanzania wametakiwa kuwa
watulivu katika kipindi hiki kinachoonekana kuwa ni cha mapasuko katika Taifa kutokana na
upotevu wa pesa ambazo ni mali
ya umma toka katika account ya Esrow.
Hayo yalisemwa na kiongozi
mmjoja wa Dini Mchungaji Eliasi Rugaganya wa Kanisa la kiinjili la Kirutheli
Tanzania Dasisi Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Betherehem Nyakato
Jijini Mwanza wakati wa Ibada ya
kipaimara iliyofanyika jana Jumapili kanisani hapo.
Rugaganya alisema kwakuwa
katika nchi yetu ya Tanzania
vipo vyombo ambavyo vinadhamana ya kuweza kushugulikia jambo hilo ni vema viachiwe kufanya kazi hiyo na
wala wananchi wasijiingize katika migawanyiko inayoweza kusababisha kuleta shida katia nchi
Aidha amevitaka vyombo vyote
husika hasa vya kisheria kufanya kazi kwa umakini na uaminifu ili kurudisha
Imani ya watanzania waliosambaratika kwa hivi sasa kutokana na kusikia kuwa
pesa nyingi kama hizo zinachukuliwa na watu wachache tena bila utaratibu huku
walio wengi wakikosa huduma za msingi katika miji na vijiji hususa ni kusuasua
kwa kwa huduma za elimu Afya na maji.
Hata hivyo alisema kuwa kwa
wale viongozi wa Dini waliotajwa katika
ripoti ya PAC hapo mwanzo kama walifanya
hivyo, na wakibainika watakuwa wameliaibisha Kanisa na kuvuruga Imani kwa
wakristo wote hapa nchini Duniani kote kwani wao ni watu wanaotegemewa sana
katika kulirejesha kanisa na wakristo wote katika uadilifu kwa kuyaacha maovu.
Alidai kuwa hata kama pesa hizo zilipitishwa kwao kwa ajili ya kufanya mambo
frani ili wabaki na zingine bado
walifanya makosa kwani ni kinyume na maadili ya Mungu hivyo ni vyema
kufuata taratibu na maadili ya Mungu ili hata wale wanaowafuata wawe waadilifu
na baadae Taifa liwe na Amani na Watu wote waishi kwa amani na Furaha kaika nchi
yao
Mwisho .
Maoni
Chapisha Maoni