Mkutano wa kilele wa Francophonie wawekwa chini ya ulinzi mkali Senegal

Mkutano wa kilele wa Francopfonie unaojumuisha nchi zinazozungumza Kifaransa unaanza Jumamosi Novemba 29 katika kituo cha kimataifa cha mikutano mjini Diamniadio, kwenye umbali wa kilomita 32 na mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Wajumbe 77, zaidi ya marais na viongozi wa serikali 40, zaidi ya wageni 5000, wakiwemo nusu ya maelfu ya waandushi wa habari wanasubiriwa katika mkutano huo ambao umewekwa chini ya ulinzi mkali.

maeneo mbalimbali ya mji wa Diamniadio na maeneo muhimu ya mji mkuu wa Senegal polisi imeimarisha usalama.
Kwa mujibu wa chanzo cha usalama, zaidi ya askari polisi 3000 wametumwa katika mji wa

Diamniadio. Kikosi cha askari pia kimetumwa katika mji huo, kwani tishio la kigaidi lipo, kama alivyoeleza Jacques Habib Sy, kiongozi wa amati ya maandalizi ya mkutano huo.
“Marais, viongozi wa serikali na wageni wajumbe wengine ambao wanashiriki mkutano huo wamelezwa hali hiyo lakini usalama umeimarishwa”, amesema Jacques Habib Sy.

Ufaransa imechangia kuimarisha usalama kwa minajili ya mkutano huo wa Francophonie. Meli ya kivita ya Ufaransa imewasili Dakar. Zaidi ya askari polisi 500, wakiwemo maafisa wa kikosi cha zima moto walipewa mafunzo na wataalamu kutoka Ufaransa katika lengo la mpango wa kuimarisha usalama wa mkutano huu ambao unaanza leo Jumamosi Novemba 29.

Hata hivyo hakuna tishio lolote kuhusu mkutano huu, kimeeleza chanzo cha usalama. Lakini tangu yalipozuka machafuko nchini Mali, Senegal inakaa kwa tahadhari kufuatia mashambulizi ya kigaidi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji