RC aipongeza Wilaya ya kibondo kwa mwendelezo wa ujenzi Maabara
KGOMA
RC aipongeza Wilaya ya kibondo kwa
mwendelezo wa ujenzi Maabara
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya ameupongeza uongozi wa wilaya ya kibondo na wananchi kwa ujumla juu ya kazi inayoendela
katika mikoa na wilaya zote hapa nchini ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari
Hayo
ameyasema leo alipokuwa akiongea kikao cha dharula cha baraza la Baraza Halmashauri wilaya ya kakonko mkoani
kigoma katika kuhamasisha ujenzi wa maabara hizo,
Machibya
amesema kuwa katika wilaya zote za mkoa huo ni wilaya mbili tu ambazo zina
uhakika wa kukamilisha vizuri ujenzi huo mnamo November 30, 2014 ambazo ni
Kigoma na Kibondo huku akizitupia lawama
zingine kuwa baadhi yao wamekuwa wakiwaachia wananchi peke yao kuwa waendelee
na ujenzi na wataalam kutokufanya kazi
zao inavyostaili
‘’
Jambo hili halitakubalika kabisa nimekuta maeneo mengine wamejenga misingi ya
tope kinyume na maelekezo alisema Machibya’’
Aidha
ameeleza kushangazwa na kitendo cha wilaya ya kakonko kukutwa haijafanya
maandalizi yoyote na kudai kuwa ni lazima ujenzi huo ukamilike muda uliopangwa
kwani maendeleo haya ni kwa ajili ya watanzania wote hata kama
serikali ndo ina hamasisha na kuwataka
viongozi wakaige mfano wilaya jirani ya kibondo ambapo wao waka kwenye hatua
nzuri za ujenzi
Nae
mkuu wa wilaya hiyo Piter Toyima amemuhakikishia kuwa muda uliopangwa ujenzi
huo utakuwa umekamilika na kwa viwango vinavyotakiwa
Machibya
alianza ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo katika wilaya zote za mkoa wa
kigoma ikiwa ni Kasulu, Kibondo Buhigwe Uvinza Kigoma vijijini na Kakonko.
Maoni
Chapisha Maoni