Raia wa India awekwa Karantini

India imemuweka karantini mwanaume mmoja ambaye alipatiwa matibabu baada ya kuathirika na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, kwa hofu kuwa huenda akasambaza virusi vya Ebola kwa njia ya kujamiiana.

Mtu huyo alipimwa na kukutwa hana virusi vya ugonjwa huo alipowasili Uwanja wa ndege wa Delhi.
Hata hivyo Maafisa wamesema amewekwa karantini kwa sababu virusi bado vilikuwepo kwenye mbegu zake za kiume ,ambapo vingeweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana.

Vifo vingi vimeripotiwa Liberia,Guinea na Sierra Leone.

Wanaume ambao hufanikiwa baada ya matibabu hushauriwa kutoshiriki kitendo cha kujamiiana vinginevyo wahakikishe wanatumia mipira ya kiume,kwa kuwa mbegu za kiume hubeba virusi hivyo kwa siku 90 baada ya kutibiwa.

Waziri wa afya wa India amesema mwanaume huyo (26) alifika nchini humo tarehe 10 mwezi Novemba.Amekuwa akibeba nyaraka zake zilizoeleza kuwa alitibiwa maradhi ya Ebola nchini Liberia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya afya, pamoja na ushahidi huo sampuli za mbegu zake za kiume zilichukuliwa na kupimwa kisha kubainika kuwa bado virusi vya ugonjwa vipo.

Wizara imesema ataendelea kubaki kwenye Karantini mpaka virusi hivyo viishe kabisa mwilini.
kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban Raia 45,000 wa India wanaishi Afrika Magharibi.
Hakuna mtu yeyote aliyripotiwa kuathiriwa na Ebola nchini India

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao