Mbunge Jimbo la Muhambwe Kizimbani kwa kuzuia uandikishaji wapiga kura
Mbunge Jimbo la Muhambwe Kizimbani kwa kuzuia
uandikishaji wapiga kura
Mbunge wa jimbo la Muhambwe mkoani kigoma Bw. Felix
Mkosamali amefikishwa katika mahakama ya wilaya ua kibondo mkoani kigoma akikabiliwa
na shitaka la kumzuia kalani muandikisha wapiga kura kuto endelea kufanya kazi
ya kuandikisha wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa katika kitongoji cha Nduta Kijiji cha kumhasha Kata ya Murungu wilayani kibondo.
Mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo, Bw. Erick Marley
mwendesha mashitaka wa polisi bw.
Peter Makala amesema tukio hilo limetokea nov.24 alipofika katika kituo
hicho nakuzuia wasiendelee kuwaandikisha wananchi na kwamba hali hiyo ni
ukiukaji wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Bw.makala amesema
kitendo cha kuwazuia wananchi hao kujiandikisha kwamba ni kuwanyima haki yao ya msingi ambapo
wananchi baada ya kuwazuia waliendelea kudai kujiandikisha lakini hata hivyo mbunge huyo alizuia kabisa
kutoendelea na kazi hiyo.
Mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo Hakimu wa mahakama ya
wilaya Bw.Erick Marley baada ya kusikiliza pande zote mbili ameiahirisha kesi
hiyo mpaka Desemb.29,2014 ambapo kesi hiyo itatajwa tena na mtuhumiwa yuko nje
kwa dhamana baada ya kutimiza masharti kwa kudhaminiwa na watu wawili kila
mmoja sh million 2 jumla yake sh million 4.
Katika eneo la mahakama hiyo ilifurika watu mbalimbali
kutoka sehemu tofauti waliofika kusikiliza kesi hiyo ambapo hali ya ulinzi ilikuwa imeimalishwa kwa kiasi kikubwa
ilikusitokee vurugu zozote pale na utulivu ulikuwepo..
Awali ilidawa kuwa Mbunge huyo alimnyang’nya kalani huyo
Vitabu na Madodoso yote na kuamua kuondoka nayo na kuyapeleka katika ofisi ya
mkurugenzi mtenda wa Halmashauri ya wilaya hiyo kinyume taratibu na baadae kukamatwa na Polisi hadi leo
aliopfikishwa mahakamani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni