MAAMBUKIZI YA VVU KIGOMA YAPANDA HADI ASILIMIA 3.4
Takwimu
za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa kigoma zinaonyesha kuwa juu kwa asilimia 3.4 kwa utafiti wa mwaka
2011 na 2012 ikilinganishwa na utafiti wa 2007/2008 ambapo maambukizi yalikua
asilimia 1.8 hali ilinayoonekana kusababishwa
muingiliano wa watu toka mikoa mbalimbali hapa nchini tofauti na miaka
ya nyuma
Hali
hiyo imetajwa kuwa utandawazi pamoja na kuiga mambo ya kisasa miongoni mwa
baadhi ya jamii za mkoa huo imekuwa ni chanzo cha ongezeko la maambukizi ya virusi
vya ukimwi kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo na uelewa mdogo
Kama
ilivyo kawaida kutokana na mila na
destuli za makabila mengi ya Tanzania,
jamii na familia nyingi hapa nchini kuna mambo ambayo si lahisi wazazi
kuwawekea wazi watoto wao kwa kuhofia uharibifu na kupelekea watoto kufikiri
mambo makumbwa zaidi ya umri hali ambayo
inawapelekea kujiingiza katika vitendo vya kufanya mapenzi bila utaratibu na
kabla ya wakati
Baadhi
ya wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa kibondo mkoani hapo, wamesema kuwa yapo
mambo mengi ikiwa ni umasikini ulevi wa pombe madawa ya kulevya kutokuwa na
elimu ya kutosha juu ya kijikinga na maambukizi katika makundi ya rika
mbalimbali na wengine kufanya makusudi hatua ambayo wameitaja kuwa wamekuwepo
wanaume ambao wamekuwa wakitumia uwezo wao wa kifedha kwa kuwarubuni watoto
wadogo wa shule za msingi na sekondari, kufanya nao matendo ya ngono bila
utaratibu kwakuwa wengi wao kutegeana na umri wao kuwa mdogo
Hayo
yamejili baada ya baadhi ya wakina dada na wakina mama wilayani hapa kuamua
kulalamika kuwa wamekuwepo baadhi ya
wanaume na vijana wa kiume kuamua
kuchana mipira ya kiume Condom,
mara msichana na mvulana au mwanaume kukubaliana kufanya mapenzi hali ambayo
imekua ikiwanya waishi kwa hofu kuwa wameambukizwa
Tatua
ielezwa katika kikao cha baraza la Madiwani cha Halmashauri ya wilaya hiyo
ambapo madiwani walisema kuwa
imewalazimu wasichana kuiomba Idara ya Afya kupitia kitengo cha ukimwi
kusambaza condom za kike ili wawe na uhuru wa kufanya mapenzi bila mashaka
Mratibu
wa kitengo cha ukimwi wilaya ya kibondo Emmanuel Makunja alipoulizwa kulikono
hadi jamii iombe mipira hiyo ya kike kwa ajili ya kujikinga na maambukizi
wakati ilitakiwa iwepo sawa na mipira ya kiume amesema kuwa kulikukuwepo na
tatizo la upatikanaji wa condom hizo lakini hivi sasa zimesha patikana na
wanataraji kuanza kuzisambaza
Kwa
upande wao baadhi ya vijana walipoulizwa na clouds, wamesema kuwa kinacho
sababisha ni uelewa mdogo juu ya kijikinga na VVU kwa kuwa vijana wengi wanadai
kuwa wakitumia mipira hiyo hawajisijii vizuri na, mtu anafanya hvyo ili yule
mpenzi wake aweze kumkumbuka siku nyingine na wengine wanafanya hivyo makusudi,
baada kujigundua kuwa wameshapata maambukizi
Nao wakina Dada na wanawake wamedai kuwa mtu
anayefanya kitendo kama hicho cha kuchana condom wakati wa kufanya mapenzi,
huyo anakuwa anajua wazi hali ya afya yake kwa
kumuambikiza mwenzake na pia mabinti
wengi uelewa wao ni mdogo ikichangiwa
na umasikini na Tamaa za vitu
vidogo vidogo
Aidha
wamesema kuwa mtu yeyote atakaye fanyiwa kitendo hicho
asikae kimya ni vizuri afike kwenye vyombo vya sheria, na akapime afya ili
kujiridhisha kama usalama kwa sababu hiyo ni aina ya unyanyapaa na kuleta athali katika maisha ya watu
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni