TRA kuwachukulia hatua wafanyabiashara

 MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wenye mitaji kuanzia sh. milioni 18 ambao hawatumii mashine za elektroniki (EFD’s) kama ilivyoagizwa na Serikali.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Meneja wa TRA Mkoa, Peter Shewiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi kanda ya Ziwa.

Shewiyo alisema hawatasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wataoshindwa kufuata kanuni na sharia ambazo zinawaelekeza kutumia mashine kwani kufanya hivyo kunakosesha serikali mapato.

Alisema endapo wafanyabishara hao watatumia mashine hizo kutawezesha kuwapungazia wizi uliyopo katika kuongeza pato la taifa na kuwanufaisha wao wenyewe katika kutunza takwimu kwa usahihi.

“Mfanyabiashara yeyote yule ambaye hatumii mashine za EFD’s haruhusiwi kufanya biashara na endapo tukimbaini mtu ambaye anaendesha biashara yake bila mashine hiyo, tutamshitaki pamoja na fidia,”alisema Shewiyo.

Naye Afisa huduma na elimu kanda ya Ziwa, Lutufyo Mtafya alisema matumizi ya mashine hizo yatasaidia kupunguza wimbi la wateja TRA na kuwasaidia kufahamu kiasi cha fedha anachodaiwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji