Changieni mfuko wa afya ya jamii mpate matibabu bora
Changieni mfuko wa afya ya jamii mpate
matibabu bora
Taifa
ili liweze kuwa na maendeleo lazima jamii iweze kujikinga na maradhi na kuwa na afya bora na kuweza kuzalisha mali kwa
ufasaha zaidi.
Kauli
hiyo imetolewa na katibu tawala wilaya ya kibondo mkoa wa Kigoma Bw, Ayubu
Sebabili wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa uchangiaji wa mfuko wa afya ya
jamii uliofanyika katika kijiji cha Bitare wilayani humo.
Sebabili
amsema kuwa jamii lazima kuhakikisha inaelimishwa kuhusu uchangiaji wa mfuko wa
afya jamii, ili iweze kuboreshewa na kupata matibabu kwa garama ndogo,
ikilinganishwa na garama za matibabu zilivyo juu sana hivi sasa, hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha
uchumi katika familia
Nae meneja wa Bima ya Afya mkoa wa kigoma Bw,
Odhiambo Eliasi amesema kuwa wananchi wakihamasishwa katika uchangiaji wa mfuko
huo, changamoto zinazoukabili mfuko huo, zitakwisha maana madawa yatapatikana
ya kutosha, kwa kuwa kiwango cha shilingi elfu 5 kwa kaya kwa mwaka ni kidogo
ambacho mwananchi anaweza kukimudu
Mganga
mkuu wa Wilaya ya Kibondo Laurian Kanegene amesema kuwa mfuko wa afya ya jamii
wilayani humo, kwa mwaka huu umefaulu kununua dawa zenye thamani ya tsh million
44 mia 224 na 500 kutoka katika Boari kuu MSD kanda ya Tabora.
Amedai
kuwa dawa hizo zitapelekwa katika zahanati zote nane na viuo vya afya viwili,
vilivyoko wilayani humo na zitagawiwa kadri rekodi za makusanyo ya uchangiaji
zilivyokwenda
Hata
hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo ambao ni Joseph Bilaza na
Vaileth Bulegea wamesema kuwa ili mfuko
huo uboreke vizuri pamoja na uhamasishaji unaoendela nilazima yafanyike kwa
wachangiaji kama kupata dawa kama utaratibu unavyoeleza watumishi kutukia luga
nzuri kwa wagonjwa.
Aidha
wameeleza kuwa kumekuwepo na usumbufu kwa wagonjwa mara wanafika kwenye
zahanati vituo vya afya na hospitali wakiambiwa kuwa dawa hazipo na kuelekezwa
sehemu kwenda kununua hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa ya kujiunga na
mfuko huo.kwani garama wanazotumia kununua madawa baada ya kuyakosa katika
mfuko huo. zinazidi zile walizochangia
Inserts
wananchi
Baadhi
ya watendaji katika sekta ya afya wamesma kuwa wao wanakabiliwa na changamoto
nyingi katika utendaji wao wa kazi, mmoja wa watendaji ambaye ni mganga wa
zahanati ya Kijiji cha Bitare Bi, Rebeca John, amesema kuwa wanakabiliwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuletewa dawa chache
zisizokidhi mahitaji kwa watumiaji hali ambayo imekuwa ikisababisha malaumu kwa
wagonjwa kuwa dawa hizo waganga wanazitumia kwa matumizi yao binafis, pia
kuuomba uongozi kuhakikisha unarekebisha hali hiyo ili mafanikio yawepo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni