Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini, chanzo ni ikiukwaji wa taratibu kwa viongozi
Mwemezi Muhingo Kibondo
Migogoro
ya wakulima na wafugaji inayoendelea
katika maeneo mengi hapa nchini, inasababishwa baadhi ya viongozi kutokuwa
elimu juu utambuzi wa migogoro hiyo, na wengine kuacha makusudi kwa kutofuata
sheria na taratibu
Akitoa
taarifa yake kamanda wa polisi wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma SP Marko Joshua.
wakati wa semina elekezi kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali na wadau wa
maendeleo, iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kibondo
amesema kuwa jamii kubwa imekuwa ikikosahaki zao za msingi kwa sababu ya baadhi
ya viongozi wasiojua na kufuata sheria kwa kuwasababishia migogoro na kugombana
wao kwa wao.
Joshua
aliesema kuwa wakulima na wafugaji wote
wanastaili haki zao kwa mujibu wa sheria za Tanzania na hatua madhubuti hazitachukuliwa
kutaingia mgogoro mkubwa ambao itakuwa vigumu kuudhibiti na kusababisha madhara
makubwa katika jamii.
‘’Halmashauri
nyingi hapa nchini hazijaona kuwa jukumu la kuhakikisha usalama katika jamii
utulivu, na ulinzi wa mali
za watu ni lao hivyo, kutotekeleza sheria namba 7 ya 1982 sheria ya serikali za
mitaa na badala yake jukumu hilo limeachiwa jeshi la
polisi peke alisema OCD Joshua’’
Hata
hivyo alisema kuwa hivi sasa serikali kuu inaelekeza huduma mbalimbali za
kijamii kwenda kwa wanannchi kupitia serikali za mitaa ili kuinua maisha yao
hivyo, moja ya majukumu ya viongozi
waliochaguliwa na wananchi kuhakikisha wanajua
matatizo yao mahitaji na kuyapatia
ufumbuzi sahihi na ikibidi kuyawasilisha kwenye ngazi za vyombo husika.
Alitanabaisha
kuwa katika maeneo ya vijijini viongozi wengi wamekuwa wakijiamulia mambo bila
kuwashikisha wananchi hali ambayo imekuwa ikizusha mitafaluku mikubwa hasa pale
wanapoona jambo linafanyika ambalo hawakuhusishwa na kwenda kuohoji ili kufahamu
taratibu zilizotumika [Comflict managemen]
Aidha
alisema kuwa wafugaji na wawekezaji wamekuwa wakikaribishwa vijijini bila
utaratibu kwakuwa wananchi ndiyo wenye maamuzi kuwa huyu aje au asije katika mikutano muu wa vijiji, na badala yake watendaji wamekuwa
wakitumia mihutasali tu tena bila kuzishirikisha idara na kamati zingine katika maeneo hayo ila wao
uamua kufanya wanavyojua na matatizo yakiishaanza,uliomba jeshi la polisi kwenda kutumia nguvu hali ambayo imekuwa
ikilisababishia lawama jeshi hilo toka katika jamii na kulichukia kwasababu ya
kutokuizuaia migogoro mapema.
Aidha alishauri kuwa ni vizuri kutambua
migogoro aina ya mgogoro, chanzo na kuzuia mapema kabla haijawa mikubwa na kuleta madhara,
kuwepo mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi, Sheria na taratibu zifuatwe,
na kujua athari zake mapema.
Kwa
upande wao baadhi ya washiriki ikiwa ni Bw, Baruani Gwimo, Mtendaji kata
Busagala na Moshi Kasase wa kijiji cha
kumukugwa, walikili kuwa matatizo mengi yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya viongozi
lakini kinachochangia ni elimu ndogo ya
kujua na kutokutambua athari na aina za
migogoro. Kingine ni kukosa maadili ya utumishi.
Maoni
Chapisha Maoni