Sierra L. kuwafidia waliokufa kwa Ebola

Wafanyakazi wa Afya huko Siera Leone
Serikali ya Sierra Leone imesema italipa dola elfu tano za kimarekani kama fidia kwa familia ya kila mfanyakazi wa afya ambaye amefariki baada ya kuambukizwa Ebola wakati akihudumia wagonjwa wa Ebola.

Kituo cha taifa cha kupambana na Ebola nchini humo kimesema fidia hiyo ya mara moja pia kwa ndugu wa wafanyakazi wa afya zaidi mia moja ambao wamekufa kwa ugonjwa huo hapo awali.

Virusi vya ugonjwa huo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini Sierra Leone ambapo katika muda wa siku tatu zilizopita zaidi ya watu mia tatu wamegundulika kuambukizwa ugonjwa huo.

Mwezi uliopita serikali ya Guinea nayo ilisema ingeanza kulipa dola elfu kumi kwa kila familia ya mfanyakazi wa afya aliyeambukizwa Ebola wakati akitekeleza majukumu yake.

Wakati huo huo Mwakilishi wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula Hilal Elver amesema zaidi ya watu milioni moja nchini Afrika ya Kati wanahitaji chakula cha msaada kutokana upungufu wa chakula uliotokana na maambikizi wa virusi vya Ebola

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao