Chibok yakombolewa na jeshi la Nigeria

Jeshi la Nigeria linasema kuwa limelikomboa eneo la Chibok siku mbili baada ya wapiganaji Waislamu, Boko Haram, kushambulia mji huo.
Wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa kutoka Chibok mwezi wa Aprili.
Msemaji wa jeshi, General Olajide Laleye, alieleza kuwa mji umekombolewa lakini alikiri kuwa operesheni bado haikukamilika na inaendelea.
Haikuelezwa hasara iliyopatikana.
Wapiganaji waliposhambulia Chibok siku ya Alkhamisi, wakaazi waliwashutumu wanajeshi kuwa walikimbia bila ya kupigana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji