Kenya kuandaa riadha ya vijana 2017

Kenya imetangazwa rasmi kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya riadha kwa vijana mwaka 2017, hiyo ni baada ya mji wa Greenboro wa Marekani kujiondoa na kuachia nafasi ya wazi nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye kusifika duniani kwa watimuaji hodari wa mbio.

Tangu awali Kenya ilianza kupata unafuu wa ushindani baada ya mji wa Bunos Aires wa Argentina kujitoa mapema.
Kenya iliwahi kuandaa mashindano ya dunia ya mbio ndefu za Cross Country mjini Mombasa mwaka 2007.

Wakati Kenya ikijiandaa kwa mashindano hayo, Uganda imeshinda ombi la kuandaa mashindano ya dunia ya mbio za Cross Country kwa mwaka 2017 baada ya kuushinda mji wa Manama wa Bahrain.

Wakati ambapo mji wa Doha Qatar wenyewe umeshinda kuwa mwenyeji wa mbio za dunia za mwaka 2019.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji