Bill Gates kusaidia kupambana na Ebola
Mfuko wa Bill na Melinda Gates
umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia
matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine
zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio.
Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi.
Mpaka sasa hakuna dawa iliyoidhinishwa wala chanjo ya kupambana na Virusi vya Ebola,matibabu ya hospitalini hutolewa kwa kuwapa wagonjwa maji ili kufunga kuharisha na dawa za kupambana na vijidudu.
Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake na namna zinavyofanya kazi.
Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF linatarajia kuanzisha majaribio ya tiba Afrika Magharibi mwezi Desemba.
Mfuko huo unamilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates na mkewe Melinda umesema kuwa utafanya kazi na washirika kadhaa kwa ajili ya kutengeneza tiba.
Tiba hiyo itatumia damu iliyotolewa na watu waliopona maradhi ya Ebola.
Akiongea mwanzoni mwa mwezi huu, Bill Gates alisema utafiti zaidi kuhusu Ebola unahitajika .
Maoni
Chapisha Maoni