BAVICHA: Serikali ijitathmini Warioba kufanyiwa fujo

BARAZA la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), mkoani Morogoro, limeitaka serikali na vyombo vyake vya dola nchini kujitathimini juu ya utendaji wake kutokana na kufumbia macho kufanyiwa fujo aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.
Katika tamko kwa waandishi wa habari lilisomwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa, Barnabas Okola, alisema tukio lililomtokea Jaji Warioba si la kufumbia macho.
"Haingii akilini kama mpaka leo vyombo vya dola nchini ikiwemo polisi wameshindwa kumkamata Paul Makonda hata kwa mahojiano tu! ni kwa namna gani inaonyesha katika suala hili kuna mkono wa viongozi hususani Mwenyekiti wa CCM…hata vyama vya siasa nchini huwa wanafanyiwa mambo kama haya," alisema Okola.
Alisema kama CCM na viongozi wake wamechoka na kujaa hofu ya kung’olewa madarakani, watafanya jambo la busara wakiondoka madarakani kwa hiari wakiiacha nchi ikiwa salama na amani, badala ya wanavyotaka kutuharibia maisha yetu.


Mwenyekiti wa Kanda, Innocent Zawadi, alisema serikali inapaswa kutambua kuwa vijana wamechoka na propaganda za kihuni, kwa hofu ya kung’olewa madarakani na kutumika vibaya kama makoleo na makarai kwenye ujenzi, akisisitiza kuwa kwa sasa kinachotafutwa ni fursa ya maisha bora.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao