Hali ya usalama yaendelea kudorora Afghanistan

Kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan, wametekeleza shambulio la bomu kwenye hoteli moja inayofikiwa na raia wa kigeni, saa chache baada ya mtu mmoja kujitoa muhanga akilenga ubalozi wa Uingereza mjini Kabul.

Watu sita wamethibitishwa kufa kwenye mashambulizi haya mawili akiwemo mwanajeshi mmoja wa Uingereza, katika shambulio ambalo ni muendelezo wa mashambulizi yanayofanywa na kundi la Taliban dhidi ya wageni na vikosi vya kimataifa.
Vikosi vya usalama nchini Afghanistan vimeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti usalama nchini humo hasa baada ya kupungua kwa askari wa vikosi vya kimataifa ambao baadhi ya nchi zimeanza kuwaondoa wanajeshi wake ikiwemo Uingereza na Marekani.
Toka kuanza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakiongoza operesheni za majeshi ya nchi za kujihami za magharibi NATO, wanamgambo wa Taliban wamezidisha mashambulizi wakiwalenga polisi na balozi za mataifa ya magharibi.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kwa sasa bado hali ya usalama nchini Afghanistan itasalia kuwa tete licha ya kuwepo kwa serikali mpya madarakani kwa kile wanachodai hakuna mpangilio mzuri wa serikali kuhakikisha wanajeshi wake wanakuwa na uwezo wa kusimamia usalama wakati huu wanajeshi wa NATO wakipungua.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji