Sekta ya viwanda yachangia 3%

 TAKWIMU zinaonesha kwamba sekta ya viwanda katika pato la Taifa imekuwa kutoka asilimia 9.8 mwaka 2010 hadi kufika asilimia 10.2 mwaka 2012, sawa na ongezeko la asilimia 0.3.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Musa, alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya siku ya viwanda, inayoadhimishwa kila Novemba 20.

Musa alisema pamoja na mafanikio hayo bado juhudi zinahitajika ili kuongeza uwekezaji hususani katika usindikaji wa bidhaa ili kuweza kukuza bidhaa hizo kwa masoko ya ndani na nje.

Alizitaja njia zitakazosaidia kuleta mabadiliko  kuwa ni pamoja na kuhawilisha teknolojia na kuwezesha utafiti wa teknolojia zitakazosaidia katika kuongeza tija.

Kuhusu maadhimisho ya siku ya viwanda, Musa alisema wameandaa maonesho ambayo yameanza jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere na yanatarajiwa kufika kilele chake Novemba 20 mwaka huu.

Naye Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI), Hussein Kamote, alisema umefika wakati sasa kwa Watanzania kuthamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

Kamote alisema pamoja na juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa katika kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa bado asilimia 70 ya Watanzania wananunua bidhaa kutoka nje.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji