‘Watanzani msinununue bidhaa kiholela mitaani’
WATANZANIA wameshauriwa kutonunua bidhaa bidhaa zisizo na uhakika wa ubora mitaani na kujikuta wakiambulia hasara baada ya bidhaa hizo kuharibika kwa kipindi kifupi.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa iStore, Vipul Shah, wakati wa ufunguzi wa duka hilo, ambalo liko katika hadhi ya juu kabisa wanayopewa wauzaji wa bidhaa za Apple ulimwenguni.
Vipul alitoa mfano kwa watanzania wanaonunua bidhaa za Apple mitaani, na mwisho hujikuta wanapata si tu bidhaa zilizo chini ya viwango au feki, lakini wanakosa huduma inayotolewa katika maduka yaliyoidhinishwa.
“Kuwa muuzaji aliyeidhinishwa na Apple katika ngazi ya juu kama hii kunamaanisha kuwa tunatambulika tupo tayari kudumisha ubora na hadhi ya bidhaa za Apple, na ndiyo maana tunachaguliwa kuwa washirika wa Apple nchini hapa,” alisema Shah.
Pia alisema kununua bidhaa kutoka kwa muuzaji aliyeidhinishwa kuna faida ya ziada, kwa kuwa bei katika maduka hayo zinafanana kote duniani.
Alisema kuwa pamoja na kuwa bidhaa za Apple zinaweza kuonekana kuwa za bei ya juu, lakini zinampa mteja thamani halisi ya pesa yake.
Aliongeza kuwa duka la istore, ambalo lina hadhi sawa na maduka ya wauzaji walioidhinishwa Amerika, Ulaya na Mashariki ya Kati, linauza bidhaa zote zinazozalishwa na Apple.
Maoni
Chapisha Maoni