Mama Maria Nyerere akerwa na wanasiasa wanaomkejeli Kikwete
FAMILIA ya baba wa Taifa, Hayati mwalimu Julius Nyerere, imetoa pole kwa Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, kwa niaba ya mama Maria Nyerere ilieleza kuwa na matumaini kwamba hali ya Kikwete inaendelea vizuri kutokana na upasuaji aliofanyiwa katika hospitali ya John Hopkins, iliyopo Baltimore nchini Marekani.
“Mimi na familia yangu tunaungana kukupa pole na tunakuombea upate nafuu kwa haraka iwezekanavyo,”
Mama Maria alisema namuombea kwa Mungu apate nafuuharaka ili aweze kurejea nyumbani salama kuendelea na majukumu yake.
Aidha mama Maria alisema anakwerwa na wanasiasa wanaomkeli Kikwete na kuwataka waache mara moja.
Maoni
Chapisha Maoni