Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2014

Katibu Mkuu Kiongozi,amemsimamisha kazi

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda , Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia , Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)”ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim...

Wapiga kura wahofia Ebola Liberia

Picha
Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia. Kura hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa vituo vya kupigia kura. Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya. Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo. Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana. Uchaguzi wa kuwachagua maseneta nchini Liberia Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya. Uchaguzi wafanyika nchini liberia licha ...

Polis FC Kibondo, kidedea dhidi ya Agent FC kwa mabao 2 - .0

Michezo Ligi ya Taifa Daraja la nne ngazi ya wilaya ilifikia tamati jana kibondo mkoani kigoma kwa kuzihusisha timu mbili za Polisi Fc na Ajent Fc amazo ndo zilifunga pazia hilo huku polisi Fc wakitoka kwa ushindi wa mawili  na Ajent Fc hawakupata kitu Wakati wa sakata hilo , polisi walipata bao la kwanza katika dakika ya 18 amabalo liliingizwa kimyani na Katusi Manumbu na goli hilo lilidumu mpaka dakika ya 45 za kipindi cha kwanza Katika hali iliyowashtua mashabiki wa timu ya Agent  katika dakika ya 60 kipindi cha pili mchezaji wa timu hiyo, Bw, Jelison Moshi,  aliipatia timu ya polis FC, bao la pili kwa kujinga mwenyewe ambapo mabao hayo yalidumu hadi dakika 90 za mchezo Timu zilizoshiriki Ligi hiyo ngazi ya wilaya ni Mbwamwitu FC, walioondoka na kombe  kwakuwa mshindi wa kwanza kwa kupata point 7, Polis FC alipata point 6, Kibondo young stars waaliapata point 3 huku mshindi wa nne akiwa ni Ajent FC point 1  Kwa mujibu wa Katibu cham...

Polisi wawili wauawa Marekani

Picha
Maafisa wawili wa polisi Eneo la mauaji ya polisi wawili mjini New York nchini Marekani Kamishna wa idara ya polisi mjini New York Bill Bratton amesema kuwa maafisa hao walilengwa na kuuawa kutokana na sare walizokuwa wamevaa. Alisema kuwa awali mwanamume huyo alikuwa ameandika ujumbe wa kuwashutumu polisi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani . Mauaji hayo ya polisi yanajiri wakati kunashuhudiwa ghadhabu kali kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa kutowafungulia mashtaka polisi wazungu waliohusika kwemye mauaji ya waamerika weusi.

Bibi amuua mjukuu wake kwa kumtupa nje ya basi kupitia dirishani

Picha
Dar/ Singida.  Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Nawaridi Saidi (45), mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kumtupa mjukuu wake Mayasa Meshack (6) kutoka ndani ya gari wakati akisafiri kwenda Kigoma akitokea Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 18, saa 2 usiku katika Kijiji cha Igugumo, wilayani Iramba ambapo mama huyo akiwa kwenye basi aina ya Scania, alifungua dirisha kutoka katika kiti alichokaa na kumtupa Mayasa wakati basi likiwa katika mwendo. “Mama alikuwa anaenda mkoani Kigoma kwa ajili ya Sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, aliambatana na mtoto wake mwingine ambaye jina bado halijafahamika,” alisema Kamanda Sedoyeka. Aliongeza: “Baada ya kumtupa mtoto huyo, abiria wenzake walianza kupiga kelele, zilizomuamuru dereva kusimamisha basi na kulirudisha nyuma ili kwenda kumwokota mtoto huyo ambaye alikuwa bado hai.” Alisema kuwa baada ya kuokotwa, mtoto huyo alipelekwa moja k...

Mwelekeo mpya; Ukawa wasema serikali ya mseto inanukia 2015

Picha
Dar es Salaam.  Matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi kote hivi karibuni yanaonyesha kuwa wananchi wamebadilisha mitazamo yao dhidi ya vyama vya siasa na hivyo kutoa picha mpya kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Uchaguzi huo uligubikwa na malalamiko katika baadhi ya maeneo nchini kiasi cha Serikali kuwaondoa kazini wakurugenzi wa halmashauri tano kwa kushindwa kuusimamia vyema, pia umevipa vyama na Serikali nafasi ya kujitafakari upya. Kwa upande mmoja, uchaguzi huo umewapa nguvu wapinzani kwa kuongeza idadi ya viti, lakini umeivuta nyuma CCM baada ya kupoteza zaidi ya nafasi 2,600 za uenyekiti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata jumla ya viti 12, 042. Vyama vya upinzani vimefanikiwa kuongeza kibindoni viti 1,981 ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka 2009 ambapo vilipata nafasi 1,230 za wenyeviti wa mitaa na vijiji. Matokeo haya yametoa mwelekeo mpya kwa vyama vya siasa ...

Umoja wa Mataifa waomba msaada kwa ajili ya Syria

Picha
Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha Dola bilioni 8.4 kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura wa kibinaadamu kwa takribani watu milioni 18 wa Syria na kuzunguka  ukanda huo unaokumbwa na mzozo. Ombi hilo limetolewa jana na maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Berlin, Ujerumani kwenye mkutano wa wafadhili na wamesema msaada huo unahitajika haraka nchini Syria, na katika nchi na jamii zinazopambana kuwahifadhi wakimbizi wa Syria. Kwa mara ya kwanza ombi hilo la Umoja wa Mataifa, linahusisha msaada wa chakula cha kuwapa nguvu na kurudisha afya, malazi, msaada mwingine wa kibinaadamu pamoja na msaada wa maendeleo. Maafisa wa umoja huo wamesema Dola bilioni 2.9 zinahitajika ili kuwasaidia watu milioni 12.2 walioko ndani ya Syria kwa mwaka 2015, na Dola bilioni 5.5 zinahitajika kwa ajili ya Wasyria walioomba hifadhi ya ukimbizi kwenye nchi jirani na zaidi ya watu milioni moja katika jamii zinazowahudumia. . Kiasi hicho cha fedha kilichoombwa mjini Berlin, ni kikubwa zaidi ya kile kilichoombwa...

Peshmerga wawajeresha nyuma IS

Picha
Operesheni ya siku mbili ya kijeshi ya wapiganaji wa Peshmerga katika jimbo la Kurdistan imefanikiwa kufungua njia kuelekea Mlima Sinjar, uliokuwa umezingirwa na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu. Mafanikio haya ni muhimu sana katika mapambano ya kuuchukuwa mji wa Sinjar, ulio chini ya mlima wenye jina hilo hilo, ambao ulichukuliwa na IS tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu. Mkuu wa Baraza la Usalama la Mkoa wa Kurdistan, Masrur Barzani, amesema vikosi vya Kikurdi vilisonga mbele jioni ya jana kuelekea kwenye mlima huo. "Leo tumekamilisha operesheni ambayo tuliianza jana, na ambayo inasimamiwa na mwenyewe Rais Masoud Barzani, ikihusisha eneo zima kutoka Zumar hadi Mlima Sinjar, kulikomboa eneo kubwa la Kurdistan, na pia kuwaokoa watu wa jamii ya Yazidi waliokwama mlimani. Ilikuwa operesheni kubwa na tunashukuru imefanikiwa," amesema kiongozi huyo. Maelfu ya Wayazidi walikuwa wamekwama kwenye mlima huo mwanzoni mwa mwezi Agosti, wakati wapiganaji wa IS walipoic...

Mahakama yawahukumu watu Sita kunyongwa hadi kufa

Picha
Dar es Salaam . Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa  washtakiwa sita  katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB. Mauaji hayo ambayo yalipata umaarufu na kupewa jina la mauaji ya Ubungo Mataa yalifanyika Aprili 20,2006  jijini Dar es Salaam. Jaji Projest Rugazia amewataja washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa kuwa ni Mashaka Pastory, John Mndasha, Martine Mndasha, Haji Kiweru,  Wycliff Imbora na Rashidi Abdikadir. Jaji Rugazia anasema aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa,  kufuatia ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa utetezi. “Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam na utambuzi wa washtakiwa kutambuliwa eneo la tukio inaonesha wazi walikuwa na nia ya kujaribu kupora takribani Sh 150 milioni mali ya benki...

JK akatisha ziara ya Pinda Uarabuni

Picha
Dubai. U.A.E Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda, hivi karibuni. Picha na Maktaba  . Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu. Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow. Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo. Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa. Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki...

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka

Picha
Dar es Salaam.  Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani w Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako  a kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini. Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa. Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya. Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 201...

Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'

Picha
Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia. Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''. Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake. Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na ...

Wanajeshi wa Nigeria wahukumiwa kifo

Picha
Mhakama moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram. Wanajeshi hao ambao walipatikana na kosa la uasi,walituhumiwa kukataa kuikomboa miji mitatu iliyokuwa imetekwa na Boko Haram mwezi Agosti. Wakili wa wanajeshi hao 54 alisema kuwa watawauwa kwa kupigwa risasi huku wengine watano wakiachiliwa huru. Wanajeshi wamelalamika kuwa hawapewi silaha na mabomu ya kutosha kupigana na Boko Harm. Kundi hilo limekuwa likipigana tangu mwaka 2009 na linalenga kujenga nchi inayoongozwa na sheria za Kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria. Zaidi ya watu 2000 wameuwawa katika mashambulizi yaliyolaumiwa kufanywa na kundi hilo kufikia sasa mwaka huu na maelfu zaidi ya watu wamelazimishwa kuhama makwao kutokana na vita vinavyoendelea. Koti hiyo ya kijeshi ilianza mwezi Oktoba na ilifanywa kwa siri.Viongozi wa kijeshi hawakupatikana kuzungumzia swala hilo. Wakili anayewawakilisha,Femi Falana,alisema kuwa wana...

Wabunge warushiana mangumi bungeni Kenya

Picha
Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya. Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria. Wabunge wa upinzani wal Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.' Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani. Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashamb...

‘Tamisemi isisimamie uchaguzi’

Dar es Salaam.  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimependekeza Sheria ya Uchaguzi Serikali za Mitaa ibadilishwe ili uchaguzi huo usimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) badala ya kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Pia kituo hicho kimetaka watendaji wa Tamisemi waliosababisha uchaguzi huo kuvurugika wachukuliwe hatua za kinidhamu. Hata hivyo, habari zilizopatikana jana jioni zilisema, Tamisemi imeshawachukuliwa hatua za kinidhamu baadhi ya watendaji wake waliosababisha kuvurugika kwa uchaguzi huo. Hatua hiyo ya LHRC imekuja baada ya kufanya uangalizi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika mikoa 25 na kubaini kasoro nyingi. Naibu Mkurugenzi wa LHRC, Ezekiel Masanja alisema makosa yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huo ni kwa sababu ya Tamisemi kutokuwa na uelewa wa masuala ya uchaguzi. Alisema kitendo cha uchaguzi kuvurugika na kurudiwa ni hasara kubwa iliyosababishwa na watendaji wazembe wa T...

Profesa Tibaijuka: sina hatia, siwezi kujiuzuru

Picha
Siku Moja baada ya kujiuzuri kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow. Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli. Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote. “Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi  kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yeyote kwe...
Picha
Bondia wa Uingereza Amir Khan ametetea taji lake la uzani wa Welterweight kwa wingi wa pointi dhidi ya bondia raia wa Marekani Devon Alexander mjini Las Vegas. Baada ya Khan mwenye umri wa miaka 28 kutawala raundi za mapema ,Alexander alitoa upinzani hafifu hadi raundi ya 8 ambapo aliweza kumpiga makonde Khan. Lakini Khan ambaye anasifika kwa wepesi wake wa kurusha makonde aliendelea kudhibiti pigano hilo huku majaji wote wakimpatia ushindi. Baadaye Khan alisisitiza mpango wake wa kutaka kuzichapa na bingwa wa dunia katika uzani huo Floyd Mayweather. ''Ninaamini kwamba nimefaulu kupewa fursa dhidi ya Bondia Mayweather baada ya ushindi huu'', alisema Khan.

Man U yaicharaza Liverpool

Picha
Kilabu ya Manchester United imeicharaza Liverpool mabao matatu bila jibu katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili. Hatahivyo ni Manchester United walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza. Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi iliopigwa na Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea. lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney. Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo. Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.

Jenerali aliyempinga Museveni arudi UG

Picha
Mwanajeshi wa Uganda ambaye alitofautiana hadharani na rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni mwaka uliopita amerejea nchini Uganda bila kutarajiwa kutoka nchini Uingereza ambapo alikuwa amekimbilia uhamishoni. Jenerali David Sejusa aliitoroka Uganda baada ya kumshutumu rais Museveni kwa kujaribu kubuni familia ya kifalme akitaka kumkabidhi uongozi mwanawe wa kiume. Sejusa pia alidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwaua watu fulani katika serikali na jeshini ambao walikuwa wakipinga mpango huo.

Zaidi ya abiria 100 wazama DRC

Picha
Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa watu zaidi ya 100 wanafikiriwa kuwa wamekufa katika ajali ya feri. Jahazi iliyojaa abiria imezama katika Ziwa Tanganyika kusini-mashariki mwa nchi siku ya Alkhamisi. Waziri wa usafiri wa jimbo hilo la Katanga, Laurent Sumba Kahozi), aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa miili kama 129 imepatikana. Inaarifiwa watu 232 walinusurika. Ajali hiyo ilitokea Alhamisi usiku kaskazini mwa jimbo la Katanga baina ya miji ya Moba na Kalemie. Waandishi wa habari wanasema ajali kama hizo zinatokea kawaida kwa sababu feri mara nyingi zinakuwa zimejaa mno.

Dunia yaambiwa isiisahau Sudan Kusini

Picha
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limeonya kuwa mwaka mmoja baada ya ghasia kuzuka Sudan Kusini mapambano bado yanaendelea baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji na kuhatarisha raia. Mkuu wa ICRC nchini humo, Franz Rauchenstein, alisema ingawa waandishi wa habari wameipa mgongo Sudan Kusini, wale walionasa katika vita hivyo haifai kuwasahau. Mapigano yalizuka Disemba mwaka jana baina ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamo wake wa rais wa zamani, Riek Machar. Watu kama milioni moja na nusu wamepoteza makaazi na mashirika ya misaada yanasema msaada wa kimataifa unahitajika kuepusha upungufu mkubwa wa chakula.

Uvunaji mazao ya mistu usiokuwa rasmi

Kibondo Tatizo la mabadiliko ya tabia nchi linaloendelea kuukabili ulimwengu limetajwa kusababishwa na uelewa mdogo wa utunzajia wa mazingira ikiwa ni pamoja na halingumu ya maisha inayopelekea watu kukata miti hovyo kwa matumizi mbalimbalikwa ajili ya biashara na kijamii katika familia Hayo yalisemwa jana na Afisa mistu wilayani kibondo mkoa wa kigoma Bw, Anod Mwambo alipokuwa akiongea na baadhi ya wakazi wa vijiji  wilaya hiyo  baada ya kuakamata vipande elf  7 vya mbao ambavyo vilivunwa kinyume cha utaratibu Mbwambo alisema kuwa hali hiyo inasababisha uharibifu wa mazingira kwa kuwa watu wasiofuata taratibu uendesha shughuli zao kwa uficho kwa kufyeka miti hovyo na kutofuata taratibu na kanuni za uvunaji hatua ambayo imefanya maeneo mengi katika wilaya ya kibondo kuwa katika hali hisiyoridhisha tofauti na hapo awali Hata hivyo alidai kuwa kama hali hiyo haitadhibitiwa mapema iwezekanavyo kutatokea hali mbaya sana ambayo wakazi wa mkoa huu hawajawahi kuku...

Chiza kufunguka sakata la uingizwaji sukari leo

SIKU moja baada ya Tanzania Daima kuripoti kuhusu sakata la sukari inayoozea katika maghala ya kiwanda cha Kilombero mkoani Morogoro, hatimaye Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhandisi Christopher Chiza, amesema leo atalitolea ufafanuzi suala hilo kwa kina. Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Chiza alisema suala la uagizaji sukari haliihusu Wizara yake tu, bali ni suala mtambuka. Kutokana na hivyo, alisema katika mkutano huo ataweza kufafanua kile kinachoendelea katika mgogoro huo, ambako waagizaji sukari na wazalishaji wa viwandani wamekuwa wakituhumiana kuhusu biashara hiyo. “Kwangu wote hawa nawaita ni wafanyabiashara na waandishi mnapaswa kuelewa hivyo, nimesoma mengi kuhusu sakata hilo na nimekuwa nikipigiwa simu na waandishi mbalimbali, hivyo nimeona ni vema nikaitisha mkutano ili kuwaeleza kwa pamoja kinachoendelea,” alisema Waziri Chiza. Pia, Tanzania Daima ilifanya juhudi za kuwatafuta waagizaji wa sukari wanaotuhumiwa kuhujumu biashara hiyo, ambako Mwenyekiti...