Kanisa Katoliki Burundi lainyooshea kidole cha lawama INEC
Kanisa Katoliki nchini Burundi, ambao lina waumini asilimia 60% kwa jumla ya idadi ya raia wa nchi hiyo na ambalo lina ushawishi mkubwa limeelezea wasiwasi wake juu yZoezi ambalolilianza wiki mbili zilizopita, limeongezwa muda wa siku tano na tume huru ya uchaguzi (Ceni), baada ya muda uliyopangwa kutamatika Jumapili Desema 7.
a kasoro zinazoendelea kujitokeza katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura
Jumapili, Desemba 7, Maaskofu wa Burundi wamelani vikali katika ujumbe kwa waumini, dosari nyingi zinazoshuhudiwa katika zoezi la kutoa vitambulisho vya uraia kwa wananchi. Upinzani na mashriki ya kiraia wamekua wakiomba zoezi hilo lisitishwe kutokana na dosari hizo, lakini tume huru ya uchaguzi (Ceni) imekua ikipuuzia wito huo.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Burundi wameamua kukemea makosa yanayoendelea katika mchakato wa uchaguzi kupitia jukwaa la kipekee, lililowakutanisha mamia kwa maefu ya waumini katika kanisa kubwa nchini Burundi la Regina Mundi. Sherehe zilirushwa hewani moja kwa moja kwenye redio ya taifa na kufuatiwa na mamilioni ya waumini. Ili kutoa uzito zaidi kwa ujumbe wao, Maaskofu wanane kutoka nchi nzima walihudhuria misa hiyo.
Ukosefu wa mazungumzo ya kisiasa, jaribio la serikali ya Burundi la kuwatenga wapinzani kwa kutumia vyombo vya sheria ... Yote hayo yanalitia wasiwasi Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Burundi. Lakini pia madai ya udanganyifu mkubwa katika zoezi la kuandika wapiga kura ndio yanazua wasiwasi zaidi kama alivyoiambia RFI mwenyekiti wa Baraza la maakofu nchini Burundi.
" Hatua ambayo tumefikia imejaa kasoro nyingi na kila mtu anatambua hali hiyo", amesema Askofu Mkuu Gervais Banshimiyubusa baada ya Misa.
Leo, mchakato wa uchaguzi nchini Burundi unaonekana kuwa hatari na Maaskofu wa Kanisa Katoliki wametoa wito kuanzisha " mazungumzo ya kweli".
" Hii ina maana kwamba kila mtu anaweza kuzungumza na kuona ni uwezekano gani halisi umbao unasalia ili tuendelea na mchakato wa uchaguzi", ameongeza Askofu Mkuu Banshimiyubusa.a kasoro zinazoendelea kujitokeza katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura
Maoni
Chapisha Maoni