Uvunaji mazao ya mistu usiokuwa rasmi

Kibondo
Tatizo la mabadiliko ya tabia nchi linaloendelea kuukabili ulimwengu limetajwa kusababishwa na uelewa mdogo wa utunzajia wa mazingira ikiwa ni pamoja na halingumu ya maisha inayopelekea watu kukata miti hovyo kwa matumizi mbalimbalikwa ajili ya biashara na kijamii katika familia

Hayo yalisemwa jana na Afisa mistu wilayani kibondo mkoa wa kigoma Bw, Anod Mwambo alipokuwa akiongea na baadhi ya wakazi wa vijiji  wilaya hiyo  baada ya kuakamata vipande elf  7 vya mbao ambavyo vilivunwa kinyume cha utaratibu

Mbwambo alisema kuwa hali hiyo inasababisha uharibifu wa mazingira kwa kuwa watu wasiofuata taratibu uendesha shughuli zao kwa uficho kwa kufyeka miti hovyo na kutofuata taratibu na kanuni za uvunaji hatua ambayo imefanya maeneo mengi katika wilaya ya kibondo kuwa katika hali hisiyoridhisha tofauti na hapo awali

Hata hivyo alidai kuwa kama hali hiyo haitadhibitiwa mapema iwezekanavyo kutatokea hali mbaya sana ambayo wakazi wa mkoa huu hawajawahi kukutana nayo hivyo jamii inatakiwa kutambua kuwa swala la utunzaji wa mazingira ni la kila mtu na kwa ajili ya vizazi vijavyo na kudai kuwa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni joto kuongezeka kwa kiasi kikubwa, mvua kutokunyesha kwa muda unaotakiwa,
Kukauka kwa mito maji kupungua kwenye maziwa na bahari na mambo mengine mengi, yanatokana na uharibifu wa mazingira.

 Hata hivyo aliwataka wananchi kufuaa taratibu za maliasili kupitia kitengo cha mistu, kwa mtu anayetaka kuvuna mazao ya mistu na kuacha kutumia njia zisizokuwa rasmi kwani akifanya shughuli zake kwa uwazi ataweza kuelimishwa  mambo mengi juu ya utnzaji wa mazingira. Ikiwa ni uchomaji mkaa na upasuaji wa mao.

Nae mkuu wa wilaya hiyo Venance Mwamoto, alisema kuwa mbao zote hizo zikusanywe ili zitumike katika ujenzi wa maabara unaoendelea katika shule za sekondari baada ya wapasuaji wa mbao kuamua kukimbilia kusikojulikana

Mwamoto alisema kuwa katika ofisi yake ipo kamati ya uvuaji wa mazao ya mistu ambapo yeye ndiye mwenyekiti wake  hivyo ni vema kwa yeyote anayetaka kufanya shuguli hizo aende apate maelekezo kwakuwa hakuna anayezuiliwa bali kila mtu afuate taratibu na sheria

Nao baadhi ya wananchi waliobahatika kuongea na Gazeti hili, ambao walitaka majina yao yasitajwe, walisema kuwa kumekuwepo na masharti magumu ambayo imekuwa ni vigumu  kuyafuata kwasababu maelekezo  ya idara ya mistu yanakwenda tofauti na utekelezaji huku wengine wakinyimwa vibali kwa makusudi


Adha alitanabaisha kuwa wapo watu wasiyokuwa na vibali ambao wanafanya biashara za mazao ya mistu ikiwa ni mkaa na mbao lakini hawachukuliwi hatua zozote hali ambayo imekuwa ikiwashangaza wengi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji