Man U yaicharaza Liverpool
Kilabu ya Manchester United imeicharaza Liverpool mabao matatu bila jibu katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili.
Hatahivyo ni Manchester United walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza.
Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi iliopigwa na Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea.lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney.
Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo.
Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
Maoni
Chapisha Maoni