Lord Coe kuwania Urais IAAF
Sebastian Coe ametangaza kuwania Urais katika shirkisho la riadha la International Association of Athletics Federations (IAAF) hapo mwakani.
Mshindi wa Olimpik mita 1500 mara mbili, kwa sasa ni makamu wa Rais wa shirikisho hilo tangu mwaka 2007.
Kwa kuongoza kikosi chake katika mashindano ya London mwaka 2012,Coe ametambulika zaidi na kuwa miongoni mwa wagombea wenye nguvu.
Lord Coe kwa sasa ametangaza waziwazi kutaka kuwania Urais wa shirikisho hilo huku akionekana kuimarika zaidi katika ushindani wa nafasi hiyo ya uongozi.
Mwanariadha huyu mwenye miaka 58 amewahi kuwa mshindi wa mbio ndefu ambapo alijipatia medali ya dhahabu mwaka 1980 na 1984.
Maoni
Chapisha Maoni