Maandamano katika miji mbalimbali ya Marekani

Maandamano yameendelea kushuhudiwa Alhamisi Desemba 4 katika miji mbalimbali ya Marekani, ambapo waandamanaji wameendelea kudai kukomeshwa ukatili 

Maandamano ya kudai mageuzi baada ya kifo cha Eric Garner, New York, Marekani, Desemba 4 mwaka 2014.
Maandamano hayo yalishuhidiwa katika miji ya New York, washington na Cleveland, wakati ambapo askari wawili waliohusika na vifo vya raia wawili weusi hawajakamatwa.
Hayo yanajiri wakati kuna taarifa ambazo zinaeleza kwamba askari polisi mmoja alimuua raia mweusi baada ya kumpokonya silaha katika jimbo la Arizona. Taarifa hiyo ilitolewa Alhamisi na polisi ya Phoenix Desemba 4 mwaka 2014.
Waziri wa sheria alifanya mkutano na vyombo vya habari kuhusu mauaji ya kijana mdogo mwenye umri wa miaka 12, aliye uawa siku 10 zilizopita katika mji wa Cleveland. Tamir Rice alikua akishikilia mikononi mwake bastola bandia ya plastiki akiwa katika eneo la michezo.
Kazi ya polisi katika mji huo imewekwa mashakani. Waziri wa sheria amesema matumizi ya nguvu na matumizi yasiyokua na utaratibu, askari polisi wasiokua na mafunzo ya kutoshapamoja na tabia sugu ya kutowaadhibu maofisa ambao hutenda makosa ndivyo husababisha visa hivyo kutokea. Waziri huyo amebaini kwamba tangu mwaka 2012 hadi 2013 visa 600 kama hivyo viliorodheshwa.
Polisi katika mji wa Cleveland imeimarisha ulinzi, ambapo manispa ya jiji na wizara ya sheria wanashirikiana kwa kujaribu kukosoa hali hio inayoikabili polisi. Tangazo hilo limetolewa ili kupunguza hasira. Hata hivhyo chama cha askari polisi wazungu wamepokea tangazo hilo kwa shingo upande. Kundi la maofisa wa polisi wazungu wamelani Alhamisi Desemba 4 adhabu kali zinazochukuliwa dhidi ya askari polisi wazungu.unaotekelezwa na askari polisi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji