Mahakama ya ICC yafuta kesi dhidi ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Kushoto ni naibu rais wa Kenya, William Ruto, akiwa na rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta ambaye kesi yake imefutwa kwenye mahakama ya ICC |
Uamuzi huu umekuja saa chache tu baada ya uamuzi wa majaji waliokuwa wanasikiliza kesi ya rais Kenyatta, juma hili kumpa muda wa wiki moja mwendesha mashtaka mkuu, Fatou Bensouda kuamua hatma ya kesi dhidi ya rais Kenyatta.
Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo miezi miwili iliyopita upande wa utetezi uliwasilisha ushahidi mahakamani ukiitaka ofisi ya mwendesha mashtaka ufute kesi dhidi ya Kenyatta kwakukosa ushahidi wa kuendelea na kesi hiyo.
Hata hivyo upande wa mashtka ulijitetea na kuiomba mahakama ikubaliane na maombi yake ya kutaka kesi hiyo iahirishwe kwa muda usiojulikana kwa kile alichodai kuwa Serikali ya Kenya imekataa kushirikiana na ofisi yake.
Juma hili majaji wa mahakama ya ICC walimpa wiki moja Fatou Bensouda kuamua iwapo ataendelea na kesi au la na kama ataendelea nayo basi aeleze kwakina ushahidi alionao kuwezesha kesi hiyo kuendelea mbele.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hili ni pigo kwa mahakama ya ICC kwakuwa ilikuwa inategemea sana ushahidi ambao haijaupata toka kwa Serikali ya Kenya na hivyo kwenye kesi hizo kubaki naibu wa rais William Ruto.Rais Kenyatta anatuhumiwa kwa ufadhili na kuchochea machafuko ya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008 ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa huku wengine mamilioni wakipoteza makazi yao.
OngeKushoto ni naibu rais wa Kenya, William Ruto, akiwa na rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta ambaye kesi yake imefutwa kwenye mahakama ya ICC |
Maoni
Chapisha Maoni