Waandaeni wananchi mapema kuwapunguzia mizigo

Viongozi wa ngazi  mbalimbali wametakiwa kuwashirikisha  wananchi wao mapema juu ya maandalizi ya shuguli za maendeleo ili kuondoa usumbufu wakati utekelezaji wa malengo yanayokuwa yamekusudiwa.

Hayo yalisemwa jana na mkuu wa wilaya  ya kibondo mkoani Kigoma, Venance Mwamoto alipokuwa akiongea wananchi wa vijiji vya wilaya hiyo,wakatia wa kukagua maendele ya ujenzi wa vyumba vya Maabara katika shule za sekondari

Mwamoto alisema kuwa wananchi wakiandaliwa mapema hususa kupewa elimu kuwa maendeleo ni kwa ajili yao  na wakashirikishwa ipasavyo, watajitoa vizuri kwa kushiriki bila kunong’ona kwa kulalamika hali ambayo italeta mafaniko katika kile kinachofanyika

Aidha alieleza kuwa   wakati wao wanakaribia kuanza ujenzi wa maabara hizo, waliamua kuanzisha Benki za Matofari katika Vijiji vyote vya wilaya hiyo ambapo wakati wa ufyatuaji wa matofali hayo kulinganana mipangilio waliyojiwekea, baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya walishiki pamoja wananchi kufanya kazi hali iliyo watia moyo wao kujituma wenyewe na kilicholeta mafanikio ni pale walipoamua kila mkuu wa Idara katika Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kupewa chumba kimoja cha maabara ili kusimamia ujenzi wake hadi kinakamilika

‘’Matofali hayohayo ndiyo tuliyatumia kwenye ujenzi wa vyumba hivyo, baada ya kukaa mwaka mmoja  hatua ambayo ilionekana kupunguza mzigo katika jamii kwakuwa mambo yaliandaliwa mapema hivyo ‘’ alisema Mwamoto.

Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa ujenzi huo umefikia hatua nzuri kwenye maeneo mengi ambapo majengo mengi yako katika hatua ya kuezekwa na mengine yanafanyiwa usafi hali mabayo inaleta matumaini ya kukamilika kwa wakati japo zipo changamoto nyingi wananchi kutokuwa na kipato cha kutosha.

Wilaya ya Kibondo ina jumla ya shule za sekondari kumi na sita, ambazo ziko kwenye mchakato wa kapata vyumba vya maabara, ambapo inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilion 1 milion 920 ambapo kwa kila chumba kimoja kinatarajiwa kutumia shilingi million 40 hadi kukamilika

Kwa upande wao baadhi ya wananchi walioweza kuongea na gazeti hili, ambao  ni Charles Leonard mkazi wa kijiji Busunzu na Paulo Rajabu mkazi wa kijiji cha kigina waliwapongeza baadhi ya viongozi walioshirikiana nao kufanya kazi japo mwanzoni kulikuwepo na changamoto nyingi kwa baadhi ya viongozi ambao walitaka kuleta unyanyasaji kupiti kivuli cha ujenzi wa maabara

Wananchi hao walidai katika kukusanya michango utaratibu uliokuwa unatumika ulitaka kuwavunja moyo lakini maelekezo yalitolewa na kulekebisha mambo yaliyokuwa tofauti na maelekezo
Mwisho


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao