Kura 153 kumwondoa Waziri Mkuu wa Somalia madarakani

Waziri mkuu wa Somalia Abdiweli Sheikh Ahmed, ameridhia kura ya bunge la nchi hiyo iliyomtaka ajiuzulu.

Katika kikao cha bunge cha jana wabunge 153 walipiga kura y akumwondoa waziri mkuu Ahmed, wakati kura 80 pekee zikitaka aendelee na uongozi.
Vyanzo vya habari vinasema kuwa kura ni sehemu ya vita vya kisiasa kati ya waziri Ahmed na raisi Hassan Sheikh Mohamud vita ambayo imeidhoofisha serikali.

Waziri mkuu wa Somali Abdiweli Sheikh Mohammed Kushoto aliyengatuliwa mamlakani
Usalama umeboreka katika nchi hiyo katika siku za hivi karibuni lakini serikali imeendelea kudhoofika na kukosa uwajibikaji.
Makundi mbalimbali yanayomiliki silaha yamekuwa yakipigana kuwania kuiongoza somalia tangu kuondolewa mamlakani kwa raisi Siad Barre mwaka 1991.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao