Mabomu manane yaokotwa Kibondo
Watu wawili waliokuwa wikichimba kifusi katika nyumba iliyokuwa ya diwani wa kata ya mabamba wilaya ya kibondo mkoa wa kigoma Bw, Ally Amin Gwanko, leo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya waganga ya kituo cha afya mabamba wameokota mabomu manane yanayosadikiwa kuwa yalifukiwa ardhini kwa zaidi ya miaka 10 katika eneo hilo
Mmoja wa wananchi hao waliokukwa wakichimba na kusogeza kifusi cha udongo ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa nyumba ya mganga katika kituo hicho, Bw fotunatus katabalo amesema kuwa yeye na mwenzake waliona vitu kama vyuma fulani ambavyo walivitilia mashaka na kumjulisha msimamizi wa ujenzi ambaye nae alichukua jukumu la kutaarifu uongozi wa kata na baadae mkuu wa kituo cha polis mabamba kutoa taarifa jeshi la wananchi JWTZ
kwa ajili ya utambuzi wa vitu hivyo kwani vitu hivyo vilikuwa vinatia mashaka
Kwa mujibu wa mtaalamu wa mabomu kutoka katika kikosi kiteule cha ulinzi wa mipakani kilichoko katika kijiji cha Nyabitaka mabamba bw damas Nyitambe amesema kuwa mabomu hayo huenda yamewekwa kadtika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 10 kwa kuwa yameonekana kuwa na kutu na kwamba kama moja lingelipuka basi yote yangeweza kulipuka na kusababisha madhara makubwa na hapa anatoa elimu kwa mamia ya watu waliofika kujionea mabomu hayo bila kujali kuwa ni hatari kwa maisha yao
Pamoja ni kwamba mabomu si kitu cha kukimbiia lakini mamia ya watu walifika kujionea tukio hilo na haya ndio yalikuwa maoni yao hali ambayo imeonyesha kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa namna ya kujikinga na milipuka hususa elimu ya kuyatambua mabomu
Kwa upende wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani kibondo bw Venance mwamoto baada ya mamia ya watu kukusanyika mahali hapo ili kuona mabomu hayo amewataka wananchi kuwa makini na kutopenda kushangaa vitu vya hatari kama hivyo kwani yanaweza kulipuka nakusababisha maafa makubwa kutokana na umati mkubwa uliofika kushangaa
Diwani huyo anahojiwa na Jeshi la polisi ili kuwa na uhakika wa swala hilo kwakuwa hapo awali ndiye aliyekuwa miliki na baadae kuiuza na ikibainika kuwa anahusika atafikishwa mahakamani kujibuma hizo.
Kumekuwepo na matukio ya mara kwa mara ya upatikanaji wa siraha za moto na mabomu katika vijiji vya wilaya za Kakonko na kibondo na mkoa mzima wa kigoma ambapo inasadikiwa kuwa yaliachwa na wakimbizi toka nchi za Burundi Rwanda na kongo walioingia Tanzania kutafuta hifadhi wakikimbia mapigano katika nchi zao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni