Kimbumbunga Typhoon Hagupit chatazamiwa kuvuma Manila

Watu watatu wameuawa na Maelfu kukikmbia makwao kutokana na kimbuga kilichotikisa nchi ya Ufilipini mwishoni mwa Juma lililopita.
Kimbuga hicho kilichopewa jina Typhoon Hagupit kinaendelea kusababisha madhara makubwa nchini Ufilipino, na kuwaacha karibu watu milioni bila makaazi.
Hata hivyo, watalaam wanasema kuwa kimbuga hiki hakifikii kile cha Typhoon Haiyan, kilichotokea mwaka uliopita nchini humo na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Mvua nyingi ikiambatana na upepo mkali unaendelea kushuhudiwa
kwa sasa katika mkoa wa Iloilo na mji wa Dolores wakati huu serikali ikisema inaendelea kuhakikisha kuwa watu wanaondolewa katika maeneo yaliyoathuriwa.
Hali ya hatari imetangazwa katika miko ya Albay, Camarines na Masbate.
Maafisa wa kutoa misaada ya kibinadamu yanasema, wanapata wakati mgumu kufikisha misaada hiyo kama chakula kwa sababu ya kuharibika kwa miundombinu kama barabara.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao