Uchaguzi Namibia mfano wa kuigwa Afrika
Chama cha Ukombozi wa Namibia SWAPO, kimeshinda kwa zaidi ya asilimia 86 ya kura za uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo. Waziri Mkuu wa sasa Hage Geingob ndiye amechaguliwa kuwa Rais mpya, huku chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1990, kikiwa kimeshinda viti vingi vya kura za ubunge.
Uchaguzi huo umeelezwa kufanyika kwa ufanisi kwa kutumia vifaa vya kielektroniki.
Ili kufahamu undani wa hali ya mambo ilivyokuwa, nilizungumza na mkazi wa mji mkuu wa Namibia Windhoek bwana Mussa Nahimana ambaye ni Mrundi mwenye kufanya shughuli zake nchini humo. Kwanza nilimuuliza, uchaguzi huo ulifanyika kwenye mazingira gani kwa kuzingatia masuala ya utulivu na usalama?
Maoni
Chapisha Maoni