TALGWU: Serikali isipolipa deni tutagomea Uchaguzi Mkuu

Dar es Salaam.

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), kimeitaka Serikali kulipa deni la Sh17 bilioni kinachodai kabla ya Desemba 31 mwaka huu, huku kikitishia kutoshiriki uchaguzi mkuu ujao ikiwa hawatalipwa.
Akitoa tamko hilo jana, Naibu Katibu Mkuu wa TALGWU, Kibwana Njaa alisema iwapo Serikali itashindwa kufanya hivyo katika muda uliowekwa, wanachama wake watagomea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Njaa alisema kwa kuwa wanachama wa TALGWU ndiyo wanaosimamia uchaguzi mkuu hivyo kutoshiriki kwao kutakuwa na athari kubwa, akiitaka Serikali kuhakikisha inalipa deni hilo ili kutokuvuruga uchaguzi.
Njaa alitoa mchanganuo wa madeni hayo kuwa ni uhamisho (Sh5.6 bilioni), likizo (Sh1.2 bilioni), matibabu (Sh450 milioni), masomo (Sh2.5 bilioni), posho (Sh2.6 bilioni) na madeni mengine ni Sh4.5 bilioni.
Katibu huyo alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kuibembeleza Serikali kwa muda mrefu bila mafanikio, huku kila mara wakiambulia ahadi zisizotekelezeka.
“Cha kusikitisha, Serikali imegeuza ni suala la kisiasa kwa kutoa ahadi zisizotekelezeka kwa kukataa kuwalipa wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kwa kuzingatia kuwa wakigoma athari zake zitakuwa kubwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, zahanati zitasimama na kwa hali ilivyo huko ndiko tunakoelekea,” alisema Njaa.
Mwaka 2013, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kulipa deni lote la wafanyakazi hao ndani ya miezi mitatu, lakini hadi sasa ameshalipa Sh7 bilioni pekee zilizotokana na malimbikizo ya mishahara.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji