Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'
Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
Maoni
Chapisha Maoni