Mugabe atarajiwa kutaja makamo mpya
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anatarajiwa kuhutubia maelfu ya wajumbe katika siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF mjini Harare.
Katika hotuba yake Bwana Mugabe anatarajiwa kutangaza nani atachukua nafasi ya makamo wa rais, Joice Mujuru, ambaye ametuhumiwa kufanya ufisadi.
Waandishi wa habari wanasema aliyeelekea kuteuliwa ni waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, lakini baadhi ya watu wanasema Rais Mugabe huenda akamteua mkewe, Grace, kuwa naibu wake.
Makamo wa rais ndiye huenda akarithi uongozi kutoka kwa Bwana Mugabe ambaye ametimia miaka 90.
Maoni
Chapisha Maoni