Sergeï Lavrov afanya ziara ya kikazi Sudani

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amefanya ziara ya kikazi nchini Sudan Alhamisi Desemba 4. Sergei Lavrov alifanya mazungumzo na rais Omar al-Bashir kabla ya kushiriki katika mkutano kati ya Urusi na nchi za kiarabu.

Moscow inataka kuimarisha uhusiano wake wa kijeshi na Sudan ambayo imetengwa na jumuiya ya kimataifa, lakini bila kuleta upinzani wowote na mataifa ya magharibi katika ukanda huo.
Urusi inaiunga mkono Khartoum ambayo inatafuta kuondokana na hali hiyo ya kutengwa. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amekutana pia na rais Omar al-Bashir , ambaye anatafutwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Mwezi Oktoba, Omar al-Bashir alifanya ziara nchini Misri na saudia Arabia. khartoum inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Libya. Jitihada ambayo imekaribishwa na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi.
Sergei Lavrov anaunga pia mkono "juhudi za rais wa Sudan kwa kutatua mgogoro wa Darfur kwa njia ya mazungumzo ya kitaifa", hata kama jeshi la Sudan linatuhumiwa kutekeleza mauaji mabaya zaidi katika eneo hilo.
"Tuna kubaliana kwamba matatizo ya ndani ya nchi lazima yatatuliwe bila kuingiliwa na mataifa mengine," amesema Sergei Lavrov, huku akibaini kwamba baadhi ya nchi zimekua zikijiingiza katika masuala ya nchi bila hata hivo kualikwa na nchi husika, na kusababisha majanga kama Iraq na Libya.
Makubaliano haya yamepelekea Moscow kufikiria kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na Sudan. Makampuni ya mafuta na madini ya Urusi yako tayari kutia saini mikataba kwa ajili ya kuanza shughuli zao nchini Sudan.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji