Vijembe vya Putin kwa mataifa ya Ulaya
Rais Vladmir Putni wa Urusi ametumia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa kushambulia mataifa ya Magharibi ambayo amesema yamekuwa na unafiki mkubwa juu ya hali ilivyo nchini Ukraine.
Bwana Putin alisema kuwa kama pasingekuwa na matatizo Ukraine wakati huu mataifa ya Magharibi bado yangalikuja na swala lingine la kujaribu kudhibiti Urusi.
Alisema pia kuwa Urusi haitakubali kusambaratika jinsi ilivyofanyika katika taifa la Yugoslavia.
Bwana Putni alisema kuwa Uchurmi wa Urusi unakabiliwa na changamoto nyingi siku za mbeleni, lakini akasisitiza kuwa vikwazo hivyo vitasaidia Urusi kuunda mbinu mwafaka za kujitegemea.
Rais aliwahimiza waekezaji kurudi tena Urusi kwa kutangaza kuwa hakutakuwepo na upekuzi juu ya uhalifu wa fedha au kama kulikuwepo na wizi wa kodi juu ya rasilmali itakayoingizwa nchini.
Maoni
Chapisha Maoni