Polis FC Kibondo, kidedea dhidi ya Agent FC kwa mabao 2 - .0
Michezo
Ligi ya Taifa Daraja la nne ngazi ya wilaya ilifikia tamati
jana kibondo mkoani kigoma kwa kuzihusisha timu mbili za Polisi Fc na Ajent Fc
amazo ndo zilifunga pazia hilo
huku polisi Fc wakitoka kwa ushindi wa mawili
na Ajent Fc hawakupata kitu
Wakati wa sakata hilo , polisi
walipata bao la kwanza katika dakika ya 18 amabalo liliingizwa kimyani na
Katusi Manumbu na goli hilo
lilidumu mpaka dakika ya 45 za kipindi cha kwanza
Katika hali iliyowashtua mashabiki wa timu ya Agent katika dakika ya 60 kipindi cha pili mchezaji
wa timu hiyo, Bw, Jelison Moshi,
aliipatia timu ya polis FC, bao la pili kwa kujinga mwenyewe ambapo
mabao hayo yalidumu hadi dakika 90 za mchezo
Timu zilizoshiriki Ligi hiyo ngazi ya wilaya ni Mbwamwitu
FC, walioondoka na kombe kwakuwa mshindi
wa kwanza kwa kupata point 7, Polis FC alipata point 6, Kibondo young stars
waaliapata point 3 huku mshindi wa nne akiwa ni Ajent FC point 1
Kwa mujibu wa Katibu chama cha mpira wa miguu Wilaya ya
kibondo Bw, James Samson wakati
wakizungumza na Gazeti hili alisema kuwa
matokeo ya mwaka huu hayana
tofauti na mwaka jana na kuwataka wachezaji wa timu zote kujikita zaidi katika
mazoezi ili kuboresha na kuinua viwango
vya uchezaji
Aidha Samsoni alisema kuwa hivi karibuni wanatarajia kwenda
mjini kigoma ili kushiriki Ligi ya mkoa ambapo mshindi wanza aliyechukua
kikombe atapewa kipaumbele, pia amewataka wadau mbalimbali wa michezo kuendelea
kujitokeza kuwaunga mkono wanamichezo wote ndani ya wilaya ya kibondo mkoani
kigoma.
Hata hivyo mmoja wa
washiriki wa mchezo wa mpira wa miguu Bw, Katusi Manumbu ambaye ni mchezaji wa
timu ya polis Fc alieleza changamoto wanazokabiliana nazo pamoja na ukosefu wa
viwanja vizuri vya kufanyia mazoezi na
michezo kwa ujumla kwani hata uwanja unaotegemewa hapa wilayani ni kokoto tupu hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tama
wachezaji wengi wakihofia kuumia
Katusi alitanabaisha kuwa timu nyingi zinakosa vifaa vya
michezo hata ushikishwaji mdogo tofauti na maeneo mengi katika mikoa mingine
hapa nchini, alisistiza kuwa katika mkoa huu wa kigoma kuna watu wenye vipaji
vizuri vya michezo hasa kabumbu wameachwa nawo wanakosa hata pa kuanzia
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni