Wanajeshi wa MONUSCO huenda wakapunguzwa 2015

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kinaweza kuwapunguza wanajeshi wake nchini humo kuanzia mwaka 2015,
Kikosi cha MONUSCO kikiwa DRC
 Mkuu wa kikosi hicho cha MONUSCO, Martin Kobler, amesema wanaweza kuwapunguza wanajeshi hao mwakani, ikiwa mamlaka ya serikali yatarudishwa mashariki mwa Kongo.
Kobler amesema kuwa tayari ujumbe kutoka New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa umeshafanya ziara katika eneo hilo kuangalia jinsi kikosi cha MONUSCO kinavyoweza kuwapunguza wanajeshi wake kutokana na kuimarika hali ya usalama kwenye maeneo mengi.
Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, ambako makundi kadhaa ya waasi wa Kikongo na yale ya kigeni yanaendelea kufanya uasi.
Mauwaji yashuhudiwa Beni
Mauwaji kadhaa yameshuhudiwa katika eneo la Beni, kaskazini mwa Kivu na watu 200 waliuawa kati ya mwezi Oktoba na Novemba. Wahanga wa mauaji hayo ni pamoja na wanawake na watoto. ya kuendelea kuwepo kwa umwagikaji damu mashariki mwa Kongo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji