Mafuriko yaleta balaa Mwanza
Mwanza.
abishwa na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa saa nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema mvua hiyo imesababisha vitu vyao kusombwa na maji na nyumba kubomoka.
Esther Misanga, mkazi wa mtaa huo, alitaja baadhi ya vitu vilivyoharibiwa na mvua hiyo kuwa ni magunia 20 ya mahindi, magunia 10 ya daga na mifuko 20 ya unga wa sembe, vyote vikiwa na thamani ya jumla ya Sh2 milioni.
“Nimepoteza magunia 50 ya mahindi na unga wa dona. Nimepata hasara kubwa sana. Sikutegemea yangetokea mafuriko makubwa kama haya,” alisema Misanga.
Alisema Serikali iliwaahidi kuwahamisha maeneo hayo kutokana na kupata adha ya mafuriko ya mara kwa mara, lakini hadi sasa utekelezaji huo haujafanyika.
“Serikali ilituahidi kutupatia maeneo kule Kisesa, lakini tangu wazungumze hadi sasa mwaka umepita hawajatuonyesha maeneo hayo. Tunaiomba Serikali ifanye kila liwezekanalo ituhamishe katika eneo hili tunusuru maisha yetu,” alisema Misanga.
Maoni
Chapisha Maoni