Mugabe awashtumu wapinzani wake chamani
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani.
Akihutubia kikao cha chama hicho, Mugabe amesema kuwa kuna majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Pia amemlaumu aliyekuwa naibu wake Joice Mujuru anayedaiwa kupanga kumng'atua na kumuita mwizi.
Chama tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusu ni nani atakayerithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ameilongoza taifa hilo tangu lijinyakulie uhuru.
Maoni
Chapisha Maoni