Bondia wa Uingereza Amir Khan ametetea taji lake la uzani wa Welterweight kwa wingi wa pointi dhidi ya bondia raia wa Marekani Devon Alexander mjini Las Vegas.
Baada ya Khan mwenye umri wa miaka 28 kutawala raundi za mapema ,Alexander alitoa upinzani hafifu hadi raundi ya 8 ambapo aliweza kumpiga makonde Khan.
Lakini Khan ambaye anasifika kwa wepesi wake wa kurusha makonde aliendelea kudhibiti pigano hilo huku majaji wote wakimpatia ushindi.
Baadaye Khan alisisitiza mpango wake wa kutaka kuzichapa na bingwa wa dunia katika uzani huo Floyd Mayweather.
''Ninaamini kwamba nimefaulu kupewa fursa dhidi ya Bondia Mayweather baada ya ushindi huu'', alisema Khan.
Maoni
Chapisha Maoni