AFCON 2015: timu 16 zawekwa katika makundi

Timu kumi na sita zitakazoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne Jumatano Novemba 3, wakati ambapo zinasalia siku chache ili michuano hiyo ianze.

Wenyeji Eqauatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ambalo linaundwa na Cote d'Ivoire , Mali, Cameroon na Uinea linaonekana kuwa ngumu zaidi ikilinganishwa na makundi mengine.
Kundi A inaundwa na Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B inaundwa na Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C inaundwa na Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D inaundwa na Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imepangwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015.
Nigeria, ambayo ni mabingwa watetezi, Angola pamoja na pamoja na Misri zilijikuta ziliondolewa katika michuano hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika michuano iliyokua ikichezwa hiviu karibuni.
Equatorial Guinea ilichukua nafasi ya Morocco, baada ya Morocco kujiengua kwenye nafasi hiyo ya kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015, ikihofia mambukizi ya virusi vya Ebola.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao